Latest Posts

PROFESA MAREKANI MATATANI KWA KUSEMA WASIOCHAGUA RAIS MWANAMKE WAPIGWE RISASI

Na Amani Hamisi Mjege.

Profesa mmoja kutoka Chuo Kikuu cha Kansas amepewa likizo baada ya video ya maoni yake darasani kusambaa sana mitandaoni mapema mwaka huu.

 

Akaunti ya Mtandao wa X ya LibsofTikTok, ilichapisha video ya profesa ambaye hajatajwa jina, akionekana akihutubia ukumbi wa mihadhara uliojaa wanafunzi, na akiwakosoa wanaume wanaokataa kumpigia kura mgombea mwanamke.

 

Kwa maneno ya moja kwa moja, anawaambia wanafunzi kuwa wanaume wanaodharau uwezo wa mwanamke kuongoza nchi wanapaswa kupigwa risasi, akidai kwamba “hawafahamu jinsi dunia inavyoendeshwa.”

 

“Kinachonikera ni kwamba kutakuwa na baadhi ya wanaume katika jamii yetu ambao watakataa kumpigia kura rais mwanamke kwa sababu hawafikiri wanawake wana akili za kutosha kuwa marais.” Alisikika akizungumza kwenye hii video.

 

Kulingana na video hiyo, profesa aligundua makosa yake mara moja. “Ondoa hiyo kwenye rekodi,” alisema kwenye video hiyo. “Sitaki wakuu wa chuo wasikie hilo.”

 

Chapisho la awali halikutaja jina la profesa huyo, lakini gazeti la wanafunzi lilimtambua kama Phillip Lowcock, mhadhiri wa sayansi ya afya, michezo, na mazoezi ya mwili.

 

Ingawa video hiyo imeenea sana hivi karibuni, chuo kikuu kilitoa taarifa ya umma kwenye jukwaa hilo, kikisema kuwa ilirekodiwa mapema katika muhula wa masomo wa chuo hicho na profesa amewekwa kwenye likizo ya kiutawala.

 

“Mhadhiri huyo anaomba radhi kwa dhati na anajutia sana tukio hilo. Nia yake ilikuwa kusisitiza utetezi wake kwa haki za wanawake na usawa, na anatambua kuwa alifanya kazi mbaya sana katika kufanya hivyo”, Kilieleza Chuo Kikuu cha Kansas,

 

Chuo hicho kimesema pia kina “mchakato uliowekwa” kwa hali kama hizi na kwamba suala hilo linachunguzwa.

 

Video hiyo ilipata umaarufu mkubwa kwenye mtandao wa X siku ya Jumatano, ambapo ilipata mamilioni ya watazamaji kutoka akaunti nyingi. Seneta Roger Marshall, kutoka jimbo la Kansas, alitoa maoni yake kuhusu kipande hicho cha video.

 

“Video mbaya kutoka kwa profesa wa Chuo Kikuu cha Kansas, mtu yeyote anayesema wanaume wasiomchagua Kamala Harris wanapaswa ‘kupangwa mstari na kupigwa risasi’ amechanganyikiwa na hapaswi kuwa karibu na wanafunzi au katika taasisi ya elimu. Ninaamini Chuo Kikuu cha Kansas kitachukua hatua za haraka na kumfuta kazi profesa huyu”, aliandika.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!