Latest Posts

PURA YAWAJENGEA UWEZO WADAU WA SEKTA YA NISHATI KUTOKA KATIKA TAASISI ZA ELIMU

MAMLAKA ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli Nchini (PURA) na wadau mbalimbali wamefanya ziara mkoani Mtwara katika visima vya gesi asilia vya Mnazi bay, Madimba na chuo cha ualimu kinachonufaika na gesi hiyo.

Ziara hiyo ina lengo la kupata elimu ya utafutaji,uendelezaji na uzalishaji wa gesi asilia kwa wadau wa elimu ya vyuo vya juu na vyuo vya kati nchini.

Akizungumzia lengo la ziara hiyo Mjiolojia Mwandamizi wa PURA, Mussa Itumbo amesema lengo kubwa ni kuwaongezea uwelewa wadau wa elimu hasa kwa wakufunzi wa vyuo mbalimbali waliyoambatana nao ili na wao waweze kuwajengea wanafunzi wao maarifa sahihi kuhusu sekta hiyo ya gesi asilia.

“Baadhi ya wanazuoni wanaohitimu kwenye vyuo hivyo wanatarajiwa kufanya kazi kwenye sekta ya mafuta na gesi hivyo kupitia elimu hii itakwenda kuwasaidia kujiandaa kwa ajili ya ushindani kwenye soko la ajira”Amesema Itumbo

 

Kwa upande wake Mdhibiti Ubora Mkuu kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Dk. Malehe Setta amesema ziara hiyo ya kuongeza uwelewa wa uzalishaji na uchakataji wa gesi asilia inakizi mahitaji ya sera mpya ya elimu kwasababu sera hiyo inahitaji kutoa elimu ambayo itawafanya wahitimu kuwa na ujuzi kuliko kutoa elimu ya nadharia pekee.

 

“Ukiangalia katika kutimiza majukumu ya sera mpya iliyoanzishwa vyuo vimeambiwa vitengeneze programu ambazo zitalenga kuwapa ujuzi wahitimu baadae hivyo kwa kufika hapa itatusaidia hasa kwa walimu kuongeza uwelewa wa namna gesi inavyozalishwa na uchakataji ambayo itaongeza thamani katika programu zao kule vyuoni .” Amesema Setta

Wadau hao walioshiriki katika ziara hiyo ni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM),Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Chuo cha Bahari (DMI),Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam(DIT),Chuo cha Teknolojia ya Ardhi (ATC), VETA MRI na wadhibiti ubora upande wa elimu ya juu na kati NACTVET pamoja na TCU.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!