Korea Kaskazini imetuma takriban puto 500 zilizosheheni takataka katika anga ya Korea Kusini katika muda wa saa 24 zilizopita, ambazo zimetatiza safari za ndege na kuwasha moto kwenye paa za majengo ya makazi, kulingana na taarifa ya maafisa wa Korea Kusini siku ya Alhamisi.
Tovuti ya The Korea Herald imeelezwa kuwa puto hizo ni sehemu ya kampeni ya propaganda inayoendelea ya Pyongyang dhidi ya waasi na wanaharakati wa Korea Kaskazini walioko Kusini, ambao mara kwa mara hutuma puto zilizobeba vitu kama vile dawa, pesa na vijiti vya USB vilivyopakiwa video na tamthilia za Korea Kusini.
Puto moja limeelezwa kusimamisha safari za ndege kutua na kuondoka Uwanja wa Ndege wa Gimpo uliopo mjini Seoul Jumatano jioni kwa saa mbili, afisa wa Shirika la Viwanja vya Ndege la Korea alisema.
Huko Gyeonggi mkoa ulio karibu na Seoul, puto lilishika moto juu ya jengo la makazi ilivyo bahati wazima moto walizima moto huo. Wanajeshi wa Korea Kusini wamesema baadhi ya puto za takataka zilikuwa na vitu vinavyoweza kusababisha moto.
“Kipima muda kimeambatishwa kwenye puto za takataka, ambazo huwa na athari ya kutoa puto na kusambaza takataka baada ya muda fulani kupita,” Lee Sung-jun, Msemaji wa Wakuu wa Pamoja wa Wafanyakazi wa Korea Kusini, aliambia mkutano”
Lee amesema maputo 480 yalitua nchini Korea Kusini kufikia Alhamisi, mengi yakiwa na karatasi na takataka za plastiki
Siku ya Jumatano, puto za Korea Kaskazini zilikuwa zimetua katika eneo la ofisi ya rais yenye ulinzi mkali mjini Seoul.