Latest Posts

RAIS SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA AFYA NCHINI -UWT

Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) imeeleza kuwa katika kipindi cha Miaka minne ya uongozi wa Rais Samia,sekta ya Afya imeboreshwa na kuimarika jambo lililochagizwa na maono na nia njema ya Rais kwa Wananchi.

UWT imeeleza kuwa imeshuhudia Mapinduzi makubwa ya uboreshaji wa miundombinu ya Sekta ya Afya kwa kiwango kikubwa katika maeneo ya Mijini na Vijijini,hali iliyochangia kupunguza vifo vya Wamama Wajawazito na watoto wachanga wenye umri chini ya miaka mitano na Wananchi kwa ujumla kupata huduma bora Afya.

Hayo yameelezwa kwenye Tamasha mapema leo Jijini Tanga la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya ‘The Global Goalkeeper Award’ inayotolewa na Taasisi ya Gates kwa Viongozi waliowezesha nchi zao kufikia malengo ya maendeleo endelevu.

Tamasha hilo lililoandaliwa na UWT limekutanisha Makundi ya Wanawake kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani likijumuisha shughuli mbalimbali ikiwemo matembezi,upimaji wa Afya bure,utoaji wa huduma za kisheria bure, uchangiaji wa damu na mambo mengineyo,ambapo mgeni Rasmi wa kwenye Tamasha ilo ni Jenista Mhagama Waziri wa Afya akiwa na Mwenyeji wake Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya UWT Zainab Khamis Shomari (MNEC).

“Mafanikio haya makubwa katika sekta hii ya Afya kama zilivyo sekta zingine imetokana na kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Rais Samia,sisi UWT Taifa tumeshuhudia mapinduzi makubwa ya Uboreshaji wa Miundombinu katika Sekta ya Afya” amesema Makamu Zainab na kuongeza

“Tumeshuhudia Ujenzi wa Hospitali za Rufaa za Kanda,Hospitali za Rufaa za Mikoa,Hospitali za Halmashauri za Wilaya 50 zilizojengwa,tumejionea ukarabati wa hospitali Kongwe,tumetembelea ujenzi wa vituo vya Afya vipya na Zahanati Mpya,Wodi za dharura,ongezeko la vitanda vya kujifungulia na mambo na zote hizi ni Juhudi za Rais Samia zilizomuwesha kutunikiwa tuzo hii”

Kwa Upande wake Waziri wa Afya Mhe. Jenista ametoa Pongezi kwa Viongozi wa Kitaifa wa UWT kwa kufanya kazi ya kuiimarisha Jumuiya na Chama Cha Mapinduzi pamoja na kuwapigania Wanawake,huku akieleza mipango ya serikali ni kuendelea kuboresha sekta ya Afya Nchini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!