Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa mkono wa Siku kuu ya Eid kwa Watu wenye mahitaji, Watoto na wazee vikongwe wanaolelewa katika vituo sita vya kulelea makundi hayo vilivyopo mkoani Tabora kwa ajili ya kusherekea siku hiyo sawa na watu wengine
Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan , Mkuu wa Mkoa wa Tabora ,Paulo Chacha na Katibu Tawala wa Wilaya ya Tabora Bi .Asha Churu wametoa salamu za Raisi kwa makundi hayo.
Kwa Upande wao, Viongozi wa vituo vilivyo patiwa mahitaji hayo akiwemo Roise Mahundi na Merry James wamemshukuru Rais Samia kuwapatia mahitaji hayo ya Sikukuu , na kwamba watasherekea kama watu wengine .