Latest Posts

RC MARA AMPOKEA DC WA BUNDA

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo amempokea rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Aswege Enock Kaminyoge aliyefika kurepoti leo baada ya kuhamishiwa akitokea Wilaya ya Maswa na kumtaka kusimamia amani na utulivu na hususan mwaka huu wa uchaguzi Mkuu.

Mhe. Mtambi amesema wakati wa uchaguzi wako baadhi ya watu wanapenda kuanzisha chochochoko na kuongeza kuwa Mkoa wa Mara hautaruhusu mtu yoyote aichezee amani na utulivu uliopo kwa sasa.

Akizungumza katika mapokezi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe.Kaminyoge amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini.

Mhe. Kaminyonge ameahidi kutekeleza maagizo hayo kwa nguvu na moyo wote na kuwaomba wananchi wa Wilaya ya Bunda wampokea na kumpatia ushirikiano.

Kwa upande wake, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vincent Naano Anney amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Mtambi kwa kufanya naye kazi vizuri kwa kipindi chote akiwa Bunda na kuahidi kufanya kazi kwa vizuri akiwa Maswa kwa maslahi mapana ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!