Serikali imetoka fursa kwa wahitimu wa Kidato cha Nne mwaka 2024 kubadilisha machaguo ya Tahasusi za Kidato cha tano na Vyuo vya kati na elimu ya ufundi kwenye mfumo wa kielektroniki wa uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga na Kidato cha tano na Vyuo.
Taarifa hiyo imetolewa Aprili 02, 2025 Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema maandalizi ya awali ya uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga Kidato cha tano na Vyuo vya Serikali Mwaka, 2025.
“Itakumbukwa kuwa Serikali imekuwa ikitoa fursa kwa wahitimu wa kidato cha nne kufanya mabadiliko ya machaguo ya Tahasusi (combination) na kozi mbalimbali walizozichagua kupitia fomu ya uchaguzi (Selform.) fursa hii huwawezesha wanafunzi kurekebisha machaguo yao kulingana na ufaulu waliopata kwenye matokeo ya Mtihani wa kidato cha nne yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).