Latest Posts

SERIKALI YAWEKA ALAMA KWENYE ELIMU YA UFUNDI KUONGEZA AJIRA

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amesema Serikali imeamua kuwekeza katika elimu ya ujuzi yaani (VETA) ili kuweza kuongeza ajira nchini kwa miaka ijayo.

Prof Mkenda amezungumza hayo mkoani Morogoro wakati wa kuadhimisha miaka minne ya dhahabu Serikali ya awamu ya sita.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana na Ajira Patrobas Katambi ameeleza Serikali ya awamu ya sita imefanya makubwa kwa vijana katika elimu,kilimo,michezo na viwanda.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Mohammed Ali kawaida amekemea vikali baadhi ya makundi ya kijamii hasa ya kisiasa ambayo yamekua yakichochea uvunjifu wa amani na uchochezi kwa jumuiya ya kimataifa ili Tanzania ikose fursa za kiuchumi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!