Shule ya sekondari Mwambisi iliyopo Kongowe wilayani Kibaha mkoani Pwani imeibuka kidedea kwa aslimia 99 katika shindano la kupanda na kutunza miti mashuleni lililoandaliwa na kudhaminiwa na Banki ya NMB nchini na kukabidhiwa hundi ya shilingi Milioni 50 ya ushindi huo.
Akitoa taarifa ya hafla ya utoaji Zawadi kwa washindi wa kampeni ya upandaji miti nchini iliyofanyika Kibaha, mkoani Pwani Mkurugenzi wa fedha wa Banki ya NMB Juma Kimori hafla iliyofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Mwambisi Kongowe wilayani Kibaha mkoani Pwani ambapo Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohammed Mchengerwa alikuwa Mgeni rasmi.
Kimori amesema NMB ilitenga Milioni 225 kwaajili ya kufanikisha zoezi hilo lililohamasisha utunzaji wa mazingira kwenye shule za msingi na sekondari nchini ambapo kila shule iliyoshiriki shindano hilo ilikabidhiwa miche 2800 ya miti waipande na kuitumza ndipo shule hiyo ya sekondari Mwambisi imekuza miche yake kwa aslimia 99 na kufanikiwa kupata ushindi wa nafasi ya kwanza nchini.
Alisema nafasi ya pili imechukuliwa na shule ya msingi Ibondo ya wilayani Sengelema mkoani Mwanza ambayo amepata shilingi Milioni 30 na shule ya sekondari Itimbo ya wilaya ya Mafinga mkoani Iringa iliyopata shilingi Milioni 20 ilichukua nafasi ya tatu.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Mohamed Mchengerwa akikabidhi hundi hizo amesema zoezi la upandaji miti na kutunza litakuwa ni moja ya kipimo cha utendaji kazi wa Wakuu wa Mikoa, makatibu tawala wa mikoa na wakuu wa wilaya wakurugenzi na makatibu Tawala wa wilaya nchini ikiwa pia ni kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais DKT ISDOR MPANGO kupanda miti milioni moja na nusu na kuitunza kwenye maeneo yao.
Aidha mchengerwa amewapongeza bank ya NMB kwa Kampeni ya miti na kusaidia serikali kutoa tuzo kwa washindi ambapo shule ya sekondari Mwambisi wameibuka washindi wa Kwanza waipokea miti elfu moja mia nane na kuipanda yoteNMB wamewapa milioni hamsini .
Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa kampeni ya upandaji miti nchini inakuwa endelevu, na kusisitiza utekelezaji wa jukumu hilo kwa ufanisi katika ngazi zote za uongozi Kutokana na umuhimu wa hifadhi ya mazingira, viongozi wote wa serikali katika mikoa, wilaya na halmashauri wanatakiwa kuhakikisha wanatekeleza maagizo hayo kwa vitendo, kwa kushirikiana na wananchi katika maeneo yao.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson Simon, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakari Kunenge, amesema miti Milioni 10 ilipandwa mwaka Jana mkoani humo na kwa mwaka huu tayari imesambazwa jumla ya Miche ya miti milioni kumi kwa ajili ya kupandwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Amesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa mkoa katika kutekeleza agizo la kitaifa la upandaji miti, ikiwa ni juhudi za kulinda mazingira na kuhakikisha mkoa unakuwa na mazingira rafiki kwa maisha na maendeleo endelevu.