Latest Posts

SINWAR KIONGOZI MPYA WA HAMAS BAADA YA HANIYE, ISRAEL YATAKA NAYE ‘AULIWE’

Kundi la wapiganaji wa Hamas limemteua Yahya Sinwar kuwa mkuu wake mpya akichukua nafasi ya Ismail Haniyeh aliyeuawa mjini Tehran juma lililopita kulingana na vyombo vya habari vya Mashariki ya Kati.

Tangu 2017, Sinwar amehudumu kama kiongozi wa kikundi ndani ya ukanda wa Gaza, sasa atakuwa kiongozi wa mrengo wake wa kisiasa.

Wakati hayo yakijiri Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Israel Katz alitoa wito siku ya Jumanne “kumuua haraka” Yahya Sinwar. Kupitia chapisho aliloliweka kwenye mtandao wa kijamii wa X, Katz amemuita Sinwar gaidi na kwamba kuteuliwa kwake kunapaswa kuwa sababu nyingine ya kuiondoa Hamas.

“Kuteuliwa kwa gaidi mkuu Yahya Sinwar kama kiongozi mpya wa Hamas, akichukua nafasi ya Ismail Haniyeh, ni sababu nyingine ya msingi ya kumuondoa haraka na kulifuta shirika hili chafu kwenye uso wa dunia”, aliandika Katz.

Hofu ya kuongezeka kwa vita vya kikanda bado inaonekana kuwa kubwa, huku Iran ikiapa kulipiza kisasi dhidi ya Israel kutokana na mauaji ya Haniyeh ambayo Israel haijatoa kauli yoyote, na Hezbollah ya Lebanon ikitishia kulipiza kisasi kutokana na Israel kumuua mmoja wa makamanda wake wakuu katika shambulio la anga huko Beirut wiki iliyopita

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!