Latest Posts

SMZ YAIPONGEZA PUMA ENERGY TANZANIA KWA KUWEZESHA MAENDELEO YAJAMII

 

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema kumekuwepo na ushirikiano mkubwa kati ya sekta za umma na binafsi katika kuchochea ukuaji wa maendeleo ya shughuli za kijamii na kiuchumi visiwani Zanzibar huku ikiipongeza Puma Energy Tanzania kwa kuzindua kituo cha kwanza cha mafuta kwa lengo la kusogeza huduma ya nishati ya mafuta kwa wananchi wote.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuzinduliwa kwa kituo cha Mafuta Cha Puma Energy Tanzania kilichopo Fuoni visiwani Zanzibar , Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar Shaib Hassan Kaduara amesema anapongeza kuzinduliwa kwa kituo hicho kwani kinaonesha dhamira ya kampuni hiyo katika kuwezesha maendeleo ya jamii.

“Kituo hiki kipya kitatumika kama kielelezo cha uwekezaji kwa siku nyingi zijazo zikionesha uwezo na ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi katika kuchochea ukuaji wa maendeleo ya shughuli za kijamii na kiuchumi hapa Zanzibar

“Nawashukuru Puma Energy Tanzania kwa uthubutu wao wa kuanza kutoa huduma ya mafuta kwa wananchi na hatua hii inakwenda kuongeza upatikanaji wa bidhaa za nishati zenye bei nafuu na bora.Kuzinduliwa kwa kituo hicho cha Mafuta cha Puma Energy Tanzania kinaendana na ajenda ya kukuza maendeleo ya usawa na kuboresha maisha ya wananchi wote wa Zanzibar .

Waziri Kaduara amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kuwa mshirika wa Puma Energy Tanzania wakati wote na kuongeza siku zote wamekuwa tayari kutathimini fursa na mipango mipya ya kuwahudumia wananchi katika sekta ya nishati.

“Hatua hii ya Puma Energy Tanzania kuzindua kituo hiki cha mafuta inaashiria hatua nyingine ya maendeleo ya sekta ya nishati Zanzibar na ni uthibitisho wa ushirikiano wenye kuleta tija kati ya Serikali na wadau wa sekta binafsi kama Puma Energy Tanzania .

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa
Puma Energy Tanzania Fatma Abdallah amesema wanekukuwa Zanzibar tangu mwaka 1994 na walikuwa wakitoa huduma ya nishati ya mafuta ya ndege lakini sasa wanazindua kituo chao cha kwanza cha kuuza mafuta ya magari na vyombo vingine vya moto.

Ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji visiwani humo na kuongeza uchumi wa Zanzibar unakuwa sana na kuongeza Puma Energy Tanzania wataendelea kuzindua vituo vya mafuta Unguja na Pemba na hiyo ni dhamira yao kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyopo Zanzibar.

Kuhusu kituo hicho , Mkurugenzi Mtendaji Fatma Abdallah amesema kimetumia zaidi ya Sh.bilioni 2.5 hadi kukamilika kwake na kimetoa ajira kwa wananchi wanaozunguka.maeneo ya Fuoni na kusisitiza kituo hicho kitatoa huduma katika Viwango vya Kimataifa.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Bodi ya Puma Energy Tanzania Dk.Selemani.Majige amesema Kampuni hiyo inajivunia ubora wa bidhaa zake na kuongeza mkakati wao kwa Zanzibar ni kuendelea kusogeza huduma zake visiwani Zanzibar.

Pia amewaomba wananchi wa Zanzibar kuendelea kuungana katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa pande zote mbili za muungano za Tanzania Bara na Zanzibar

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!