Latest Posts

ST. JUSTIN YAWAIBUA WATOTO 264 WENYE ULEMAVU WALIOKUWA WAMEFICHWA MUSOMA

 

Watoto takribani 264 wenye ulemavu katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Mkoani Mara waliokuwa wamefichwa bila kuanza masomo wameibuliwa kutoka majumbani katika kata Sita za Bugwema, Nyambono, Ifulifu,Nyakatende,Mgango na Nyegina kisha kuandikishwa kuanza masomo.

 

Akitoa Taarifa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya pinga Ukatili na chochea ujumuishaji watoto na Vijana wenye ulemavu mratibu wa Mradi kutoka St. Justin Stephenano Ariyo Alisema kata ambazo zimebainika kuwa na watoto hao nipamoja na Mugango,Nyakatende, Nyambono,Bugwema,Ifulifu,pa.oja na Nyegina.

 

Pia alisema baada ya kuibuliwa watoto hao kutoka majumbani tayari wameshaanza masomo kuhakikisha wanatimiza na kuzifikia ndoto zao huku wakazi wa Maeneo husika wakitakiwa kutofawacha watoto hao.

 

Kwa upande wake mkurugenzi wa St Justin Foundation Sister Juliana Kitela ameitaka jamii hasa wanaume kuwatunza na wakuwatimizia haki zao za Msingi watoto wenye ulemavu badala ya kuwachia mzigo huo wanawake Pekee.

 

“Kwenye malezi tunawajibu wakulea wote wapo wakina Baba wamekuwa wakiwaachia majukum haya wanake tuwaombe Sana saidieni katika hili msijitoe”Alisema sister Juliana Kitela mkurugenzi St Justin Foundation.

Aidha naye Bwana Ruge Kelvin ambaye akimwakilisha Mkurugenzi amewaagiza watendaji wa kata na Vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma kuanza kuwabaini watoto wote wenye mahitaji Maalum ambayo hawajaanza masomo kisha kuhakikisha wanapelekwa shule.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!