Latest Posts

SUNGUSUNGU WAONYWA KUTUMIA MAMLAKA VIBAYA

Jeshi la jadi (Sungusungu) wameonywa kuacha kutumia nguvu au mamlaka yao kupitiliza pindi inapotekea mtu kufanya mambo yasiyothibitika kwa mujibu wa Sheria.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Tawala Mwandamizi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mashaka Makuka amesema wakati mwingine Sungusungu wamekuwa wakitoa amri kwa watu wanaosadikika kuwa na imani za kishirikina kuondoka ndani ya masaa 24 jambo ambalo ni kinyume cha sheria na haki za binadamu.

Hata hivyo Makuka amesema pia Sungusungu wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi kwa kuharibu au kuchoma mali za mtuhumiwa pasipo kujiridhisha na kumfikisha katika vyombo husika.

Akiunga mkono hoja hiyo Mkufunzi wa Elimu ya Uraia na Utawala Bora kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, Iddah John amewataka Sungusungu kuacha kutoa adhabu kubwa kwa mtu anayebainika na makosa katika jamii na badala yake wamfikishe kwenye vyombo husika.

Mbali na Sungusungu pia Iddah amekemea kitendo cha baadhi ya viongozi wa kijamii kuwapa adhabu kubwa kuliko uwezo wao watu wanaofanya makosa kwenye jamii mfano kutokuhudhuria misibani, vikao au shughuli za kijamii.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!