Latest Posts

TAASISI ZA KIMATAIFA ZAALIKWA KATIKA SEKTA YA MAJI TANZANIA

Taasisi za kimataifa zimealikwa nchini Tanzania katika Sekta ya Maji na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandiai Mwajuma Waziri.

Taasisi hizo ni pamoja na WaterAid, UNICEF, NDC Partnership na Climate Action Network Tanzania hasa katika kushirikiana na Serikali katika kutekeleza malengo ya maji katika Mpango wa Taifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (Nationally Determined Contribution -NDC) unaotekelezwa chini ya Makubaliano ya Mkataba wa Paris kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (Paris Agreement 2015).

Mhqndisi Mwajuma amealika wadau hao wa maendeleo akifungua warsha kuhusu utekelezaji wa malengo ya maji na afya katika Mpango wa Pili wa Mabadiliko ya Tabianchi (Nationally Determined Contribution) wa mwaka 2021-2025 pamoja na maandalizi ya Mpango wa Tatu wa Mabadiliko ya Tabianchi (Nationally Determined Contribution) wa mwaka 2025-2030.

Warsha imebainisha fursa ya kuongeza ufadhili wa fedha kupitia wadau mbalimbali katika uandaaji na utekelezaji wa Mpango wa Nationally Determined Contribution awamu ya tatu kuanzia mwaka 2025.

Hayo yamejiri katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) unaofanyika Jijini Baku nchini Azerbaijan ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Philip Isdor Mpango anaongoza ujumbe wa Tanzania.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!