Latest Posts

TAMWA YATETEA USALAMA MTANDAONI KWA WANAHABARI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimeendeleza juhudi za kuimarisha uwezo na ufanisi wa waandishi wa habari kwa kuwawezesha kujilinda dhidi ya vitisho vya mtandaoni, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Akizungumza siku ya Alhamisi wakati wa mafunzo maalum yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Dkt. Rose Reuben, amesema mafunzo hayo yanawapa waandishi mbinu za kuhakikisha usalama wao binafsi na wa taarifa wanazozisambaza katika majukwaa ya kidijitali.

Amesema usalama wa waandishi wa habari ni sehemu muhimu ya kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unafanyika kwa ufanisi na kwa uadilifu. Ameongeza kuwa waandishi wanapokuwa salama, wanaweza kuandika kwa uhuru na kwa weledi.

Amebainisha kuwa TAMWA inalenga kuwalinda hasa waandishi wa habari wanawake ambao mara nyingi hukumbwa na mashambulizi ya mtandaoni yanayohusisha lugha chafu, vitisho na unyanyasaji wa kijinsia.

Mafunzo hayo yamegusia mambo muhimu ikiwemo namna ya kutambua na kukabiliana na mashambulizi ya mtandaoni, matumizi salama ya mitandao ya kijamii wakati wa uchaguzi, uandishi unaozingatia maadili, ukweli na kuepuka habari potofu

Dkt. Rose pia alikumbusha wajibu wa wanahabari kutumia majukwaa ya kidijiti kwa busara na weledi, ili kusaidia kulinda amani, hususan wakati huu nyeti wa uchaguzi.

Washiriki wa mafunzo hayo waliishukuru TAMWA kwa kuandaa programu hiyo wakisema imewajengea uwezo wa kiusalama na kisaikolojia, na kuwapa nyenzo za kuepuka mashaka wanapotekeleza majukumu yao ya kitaaluma kipindi cha uchaguzi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!