Latest Posts

TANROADS PWANI YAADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU KWA KUFANYA USAFI NA KUPANDA MITI TUMBI

 

Na Mwandishi wetu Kibaha

WAFANYAKAZI wa Wakala ya Babara (TANROADS) Mkoa wa Pwani wameshiriki maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru kwa kufanya shughuli za Usafi wa Mazingira na kupanda miti katika Hospitali teule ya Rufaa Mkoa wa Pwani ya Tumbi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Meneja wa TANROADS Mkoa wa Pwani Mhandisi Baraka Mwambage amesema utekelezaji wa shughuli hizo ni kuunga mkono maelekezo ya Serikali ya kufanya shughuli za kijamii katika maadhimisho hayo.

Amesema kwa taasisi yao wameungana na utaratibu wa ngazi ya Mkoa kufanya Usafi katika Hospitali hiyo sambamba na kupanda miti kutunza mazingira.

Mhandisi Mwambage ameeleza kwamba kila mwaka TANROADS wamekuwa na utaratibu wa kufanya shughuli za kijamii kwenye juma la maadhimisho jambo ambalo wamefanya pia kwa mwaka huu.

Afisa Rasilimali watu wa TANROADS Mkoa wa Pwani Pamela Mchonde amesema shughuli walizozifanya katika maadhimisho hayo ni za kimazingira ambazo wananchi wanatakiwa kuiga na kiuzifanya bila kusubiri wakati wa maadhimisho.

Mchonde amesema Jamii inatakiwa kutunza mazingira muda wote na kuachana na tabia ya kukata miti ovyo ambayo inachangia mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa upande wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Katibu Tawala wa Mkoa huo ambae pia ni Skauti Mkuu Tanzania Rashid Mchatta ameongoza wakuu wa idara na watumishi wengine kufanya Usafi na kupanda miti katika Hospitali hiyo.

 

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!