Latest Posts

TEA YAKAMILISHA UJENZI WA MATUNDU 24 YA VYOO SHULE YA MSINGI LIKUNJA, RUANGWA

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imekamilisha ujenzi wa matundu 24 ya vyoo katika Shule ya Msingi Likunja, iliyopo wilayani Ruangwa mkoani Lindi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia nchini. Shule hiyo ina jumla ya wanafunzi takribani 470 ambao awali walikabiliwa na uhaba mkubwa wa vyoo, hali iliyokuwa ikiathiri ustawi wa wanafunzi, hususan katika masuala ya afya na mahudhurio ya darasani.

Ujenzi wa vyoo hivyo umezingatia mahitaji ya wanafunzi wa jinsia zote, kwa kujenga matundu yaliyotenganishwa kati ya wavulana na wasichana ili kutoa hifadhi na faragha stahiki, hasa kwa watoto wa kike. Mradi huo umetekelezwa chini ya ufadhili wa TEA ikiwa ni utekelezaki wa mkakati wake wa kuimarisha miundombinu ya elimu, kwa lengo la kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji hapa nchini.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vyoo hivyo, Kaimu Mkurugenzi Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi wa TEA Bw. Masozi Nyirenda alieleza kuwa, mradi huu ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kuhakikisha kila mtoto anapata elimu katika mazingira bora, rafiki na salama. Alitoa wito kwa uongozi wa shule na jamii kuvitunza vyoo hivyo ili viweze kuhudumia wanafunzi wengi zaidi kwa muda mrefu na kwa ufanisi.

Uongozi wa Halmashauri na kamati ya Shule ya Msingi Likunja waliipongeza TEA kwa mchango huo mkubwa, wakieleza kuwa mradi huo umeleta faraja na matumaini mapya kwa jamii. Wameahidi kushirikiana katika kuyatunza matundu hayo ya vyoo, huku wakitoa rai kwa taasisi nyingine kuiga mfano wa TEA katika kusaidia maendeleo ya elimu nchini kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!