Latest Posts

TEF YAMPAONGEZA MACHUMU, TIDO MHANDO KUTEULIWA NA RAIS SAMIA

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limewapongeza Dk. Bakari Steven Machumu na Tido Mhando baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kushika nyadhifa muhimu za mawasiliano Ikulu.

Bw. Machumu, ambaye hadi uteuzi wake huu unamkuta, alikuwa Makamu Mwenyekiti wa TEF ambapo ametajwa na jukwaa hilo kuwa mmoja wa viongozi waliotoa mchango mkubwa katika kuimarisha ushirikiano kati ya wahariri na wadau wa habari nchini.

Kupitia taarifa kwa umma ya Jukwaa iliyotoleq na Mwenyekiti wake, Deodatus Balile, TEF imemwelezea kama mchapakazi, mwenye weledi, uzoefu mpana na uwezo wa kiutawala unaoendana na mahitaji ya mawasiliano ya Serikali.

Kwa msingi huo, TEF inaamini kuwa uteuzi wake kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu utaongeza ufanisi katika mahusiano kati ya Ikulu na sekta ya habari

Katika uteuzi mwingine, Rais Samia amemteua Tido Mhando kuwa Mshauri wa Rais, Habari na Mawasiliano.

TEF imemwelezea Mhando kama mwanahabari mkongwe na mwenye uzoefu mpana unaohitajika katika mazingira ya sasa yanayokabiliwa na changamoto mbalimbali za kidijitali na kimataifa za mawasiliano.

TEF imeeleza kuwa kwa uzoefu na umahiri wa viongozi hao wawili, taifa linatarajia kuona maboresho katika utoaji wa taarifa za Serikali kwa wananchi pamoja na kuimarika kwa mifumo ya mawasiliano ya umma.

“Tunawatakia kila la heri katika majukumu yao mapya. Tunaamini watatoa mchango mkubwa katika kuboresha mawasiliano ya Serikali,” imesema taarifa hiyo iliyosainiwa na Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!