Latest Posts

TISHIO KIPINDUPINDU MBEYA DC, KAIMU DED AHIMIZA USAFI

NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Halmashauri ya Mbeya mkoani Mbeya imearifu kuwepo kwa ugonjwa wa kipindupindu hivyo kuwataka wananchi kuchukua hatua za usafi ili kuepukana na kuenezwa kwa ugonjwa huo.

Pamoja na kutoainisha ni wagonjwa wangapi waliokumbwa na ugonjwa huo, Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mbeya Gideon Mapunda, amesema ugonjwa huo umefika katika baadhi ya kata za wilaya ya Mbeya.

Kufuatia taarifa hiyo, amewataka wananchi kuchukua tahadhari juu ya kutoenea zaidi kwa ugonjwa huo kwa kuhakikisha wanasafisha mazingira yanayowazunguka, kunawa mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji safi yanayotiririka, kunywa maji yaliyochemshwa na kuhakikisha wanaepukana na uchafu kwa ujumla na kuwataka watendaji wa vijiji na kata kusimamia usafi kwenye maeneo yao.

Amesema hayo wakati akizungumza kwenye ibada ya kuaga mwili wa marehemu Joramu Jilla ambaye ni baba mzazi wa Lameck Jilla katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Mbeya vijijini yaliyofanyika Desemba 12, 2024 katika kijiji na kata ya Isuto wilayani Mbeya.

Naye mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mbeya vijijini Akimu Mwalupindi, ameitaka Halmashauri hiyo kuhakikisha wanakomesha uenezwaji wa kipindupindu ambacho kimeripotiwa wilayani kwake ikiwemo kwa watoto mashuleni ili kuwalinda na magonjwa ya mripuko.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!