Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Kanda ya Mashariki yasherehekea sikukuu ya Uhuru kwa kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kula na watoto waliopo mahabusu ya watoto na kuwapelekea zawadi mbalimbali Kisutu jijini Dar es salaam.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania-TPHPA Prof. Joseph C.Ndunguru, kaimu Meneja Kanda ya Mashariki Dkt.Mahamudu M.Sasamalo amewasilisha zawadi mbalimbali kwenye kituo cha mahabusu ya watoto kilichopo Kisutu jijini Dar es salaam.
Katika kusherehekea sikukuu ya Uhuru watumishi wawakilishi wa Kanda ya Mashariki walipata chai ya pamoja na watoto hao.
kisha kukata keki ya miaka 63 ya Uhuru, kugawa zawadi mbalimbali na baadae kushiriki zoezi za kupanda miti. Jumla ya miti 63 ya matunda mbalimbali yalitolewa kuashiria miaka 63 ya Uhuru wa Nchi yetu.
Katika hafla fupi hiyo mambo mbalimbali yaliyofanyika ikiwa ni pamoja na zoezi la upandaji miti ni muendelezo wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kututaka wananchi kupanda miti ili tuweze kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi,
” Tumegawa miche ya matunda ili itupatie faida mbalimbali kama kutupatia kivuli, matunda, hewa safi na kupunguza joto.”
AKISEMA Kaimu Meneja wa Kanda ya Mashariki ambae amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA Prof. Joseph C. Ndunguru.
TPHPA ni sehemu ya jamii, hivyo ni wajibu wetu wa kuwa karibu na jamii katika matukio mbalimbali, kwani miongoni mwa jukumu la TPHPA ni kulinda Afya ya Binadamu, wanyama na mazingira.
Meneja wa kituo hicho Ndugu Delius aliomba Mamlaka kuendelea kuwa sehemu ya faraja kwa watoto hao kwa kushiriki matukio mbalimbali kama siku ya mtoto wa Africa na mengineyo.