Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa imeendelea na kampeni yake ya kutoa elimu ya kodi kwa wanafunzi kwa kutembelea shule tatu za sekondari katika wilaya ya Kilolo.
Katika ziara hiyo, TRA imejionea jinsi klabu za kodi shuleni zinavyofanya kazi, huku ikiwasisitiza wanafunzi kuwa mabalozi wa elimu ya kodi katika jamii zao.
Meneja wa TRA wilaya ya Kilolo, Likweza Dindili, amewahimiza wanafunzi kutumia klabu hizo kuelimishana juu ya umuhimu wa kodi na kuhakikisha wanadai risiti kila wanapofanya manunuzi.
Shule zilizotembelewa ni Sekondari ya St. James, Sekondari ya Udzungwa, na Sekondari ya Kilolo, zote zikiwa wilayani Kilolo, mkoani Iringa.