Latest Posts

TRA WATOA MSAADA WENYE THAMANI YA MIL.5 SHULE ZENYE MAHITAJI MAALUM 

 

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA Mkoa wa Mtwara katika kusheherekea kilele cha wiki ya shukrani kwa mlipa kodi wametembelea Shule mbili za Msingi zenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii na kutoa msaada wa viti na meza vyenye thamani ya shilingi milioni 5.

 

Shule walizotembelea ikiwemo shule ya Msingi Shangani kwa watoto wenye utindio wa ubongo ambayo imekabidhiwa meza 6 kila meza moja inatumiwa na watoto 4 na viti 24 vyenye thamani ya shilingi milioni 2,020,000

 

Pia shule ya msingi Rahaleo kwenye watoto viziwi na mabubu wamekabidhi meza 7 ambapo kila meza moja watatumia watoto 6 na viti 42 vyenye thamani ya shilingi milioni 2,980,000 ambapo shule hizo zote zipo kwenye ni katika Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Aidha zoezi hilo limeendeshwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Mtwara, Maimuna Khatibu ambapo ameeleza kuwa msaada huo umelenga kuthamini jitihada za walipa kodi na kurudisha kwa jamii.

 

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani…………

… ametoa wito kwa wazazi na jamii kwa ujumla kutowafungia ndani watoto wenye ulemavu badala yake wawapeleke shule wakajumuike na wengine na kupata elimu itakayowasaidia.

 

Pia amewapongeza TRA kwa msaada walioutoa na kuwataka wafanyabiashara kwenye manispaa hiyo kuendelea kulipa kodi kwa wakati ili jamii izidi kunufaika na kodi hizo.

 

Kwa upande wao walimu wakuu wa shule hizo wamewaomba wadau wengine kuiga mfano huo kwani mahitaji bado ni mengi kwa watoto wenye mahitaji maalum ikiwemo malazi,usafiri pamoja na chakula.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!