Latest Posts

TRUMP AKIRI: HAKUNA MAFANIKIO MAZUNGUMZONI NA PUTIN KUHUSU UKRAINE

Rais wa Marekani Donald Trump amesema hakufanikiwa kufikia makubaliano yoyote kuhusu kusitisha mapigano nchini Ukraine baada ya kufanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Kambi ya Jeshi la Anga ya Andrews, mjini Washington, Trump amesema walizungumzia mgogoro wa Ukraine na hali ya Mashariki ya Kati, lakini hakuna hatua madhubuti iliyopatikana katika kuzuia vita vinavyoendelea.

“Hapana, sijapata mafanikio yoyote katika mazungumzo naye,” amesema Trump alipoulizwa iwapo alikaribia makubaliano ya kusitisha mapigano.

Kwa mujibu wa msaidizi wa Putin, Yury Ushakov, mazungumzo hayo yalichukua takribani saa moja, na yalijikita katika hali ya kijeshi nchini Ukraine pamoja na ushawishi wa Marekani katika usambazaji wa silaha.

“Mazungumzo yalikuwa ya wazi, ya moja kwa moja na thabiti,” alisema Ushakov, akiongeza kuwa Putin alisisitiza msimamo wa Urusi kutolegeza masharti yake katika mzozo huo.

Aidha, viongozi hao wawili wamejadili hali ya Iran na Mashariki ya Kati kwa ujumla. Ushakov pia alithibitisha kuwa mazungumzo yajayo ya Istanbul kati ya Urusi na Ukraine yataendelea kuwa ya pande mbili bila ushiriki wa Marekani.

Rais Putin alitumia mazungumzo hayo pia kumpongeza Trump kwa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Marekani, inayosherehekewa Julai 4 kila mwaka.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!