Latest Posts

TSHISEKEDI KUBADILI MSIMAMO? DRC KUKUTANA NA M23 ANGOLA

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imetangaza kutuma ujumbe wake nchini Angola siku ya Jumanne kwa ajili ya mazungumzo ya kusuluhisha mzozo dhidi ya waasi wa M23, kundi linalodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, ofisi ya rais wa DRC ilisema Jumapili.

Angola ilitangaza wiki iliyopita kuwa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya DRC na waasi wa M23 yataanza Machi 18 jijini Luanda.

Rais Felix Tshisekedi, ambaye kwa muda mrefu amekataa kuzungumza na waasi wa M23, anaonekana kubadilisha msimamo wake kutokana na kupungua kwa uungwaji mkono wa kikanda kwa serikali ya Kongo.

Msemaji wa M23 Lawrence Kanyuka alitangaza kupitia X (zamani Twitter) kuwa kundi hilo limekubali mwaliko wa Angola, lakini hakuthibitisha ikiwa litatuma wawakilishi wake.

Baada ya kutangazwa kwa mazungumzo hayo, M23 imeweka masharti kadhaa, ikiwemo kutaka Rais Tshisekedi atoe tamko rasmi kuhusu dhamira yake ya kujadiliana nao moja kwa moja.

Angola imekuwa ikijaribu kupatanisha mvutano kati ya DRC na Rwanda, huku Kigali ikikanusha madai kwamba inaunga mkono M23.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!