Latest Posts

TUNDU LISSU SIO MHAINI, NI MTETEZI WA HAKI ZA BINADAMU: MWAIKAMBO

 

Na Josea Sinkala, Chunya Mbeya.

Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya mafunzo wa CHADEMA kanda ya Nyasa Chance Mwaikambo, amesema kitendo cha jeshi la Polisi kutaka kuzuia wananchi kwenda kusikiliza kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu ni kukisaidia Chama Cha Mapinduzi kuendelea kusalia madarakani na kutaka wanachama kujitokeza kwa wingi mahakamani Aprili 24, 2025.

Amesema hayo wakati akizungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari kuelekea kusikilizwa kwa shauri linalomkabili mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Antipas Lissu ambapo ameeleza kuwa nchi haina utulivu kutokana na matendo yasiyofaa ya utekaji na mauaji nchini pamoja na kukabiliwa na sheria za kiuchaguzi zinazodaiwa kuipendelea CCM kwa kuwa pia na tume ya uchaguzi ambayo sio huru.

“Mimi ndiye nitaongoza wanachama wa CHADEMA kutoka Chunya kwenda kusikiliza kesi ya mchongo ya mwenyekiti wetu Taifa Mhe. Tundu Lissu, hawa CCM wnaaogopa uchaguzi wangekuwa hawaogopi wasingekuwa wanatengeneza kesi za mchongo”, amesema Mwaikambo na kuongeza;

“Tunavyozungumza hivi wako ndugu zetu wengi wamepotea hatujui wako wapi halafu bado kuna watu wanaona twende kwenye uchaguzi kwa mazingira ya sheria hizi za Tanzania haiwezekani”, ameeleza Chance Mwaikambo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!