Latest Posts

TUNGEKUWA MAWAKALA WA CCM TUNGEKUWA NA MA-V8; MWENEZI CHAUMMA

 

 

Na Josea Sinkala, Mbeya.

 

Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Taifa, kimeitaka Serikali kusikiliza maoni ya wananchi kwa kuruhusu kupatikana kwa katiba mpya itakayozaa time huru ya uchaguzi badala ya kuwa na wasimamizi wa uchaguzi ambao wanatokana na Serikali na Chama tawala (CCM).

 

Hayo yameelezwa na katibu wa habari na uenezi wa Chama Cha Ukombozi wa Umma Tanzania (CHAUMMA) Taifa Ipyana Samson Njiku, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya kuhusu msimamo wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

 

Mwenezi huyo wa CHAUMMA Taifa, amesema chama hicho kimejipanga na kinaendelea kujiandaa ipasavyo kuhusu uchaguzi mkuu bila kutegemea usaidizi wa Chama kingine chochote.

 

Amesema CHAUMMA inaendelea kuitaka Serikali kuruhusu mchakato wa upatikanaji katiba mpya na tume huru ya uchaguzi akidai tume ya uchaguzi imekuwa na watu ambao wanatokana na chama tawala hivyo mapendekezo ya CHAUMMA ni viongozi na makamishna wa tume huru ya uchaguzi wapatikane kwa ushindani badala ya kuteuliwa pekee.

 

Aidha katibu huyo wa idara ya habari na uenezi Taifa amekanusha madai ya kuwa CHAUMMA inashirikiana na Chama tawala CCM.

 

“Sisi CHAUMMA tumejipanga na tuko imara sisi wenyewe, hatuwezi kushirikiana na vyama vingine na havijatujulisha chochote, sisi tuna katiba yetu wenyewe, tuna usajili lakini tunasikia watu wanasema sisi ni kama tawi la CCM nataka kukanusa sisi hatushirikiani nao, tungekuwa na ushirikiano na CCM si hata tungekuwa na ma-V8 (magari ya kifahari) kwahiyo sisi tunajitegemea, hata hapa kuja kuzungumza na waandishi wa habari hatujatumwa na mtu yeyote”, ameeleza Ipyana Samson Njiku, katibu mwenezi wa CHAUMMA Taifa ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Mbeya.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!