Latest Posts

UKRAINE IKO TAYARI KUSITISHA MAPIGANO KWA SIKU 30, MAREKANI YATANGAZA MPANGO MPYA

Ukraine imesema iko tayari kusitisha mapigano na Urusi kwa siku 30, hatua inayokuja baada ya mazungumzo ya amani kati ya Marekani na Ukraine yaliyofanyika nchini Saudi Arabia.

Mpango huo umetangazwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, ambaye amesema kuwa sasa mpira uko mikononi mwa Urusi, akimaanisha kuwa ni juu ya Moscow kuamua ikiwa itakubaliana na pendekezo hilo.

Katika hotuba yake, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameeleza kuwa ni jukumu la Marekani kuishawishi Urusi kukubaliana na mpango huo, akiuona kama fursa muhimu ya kupunguza ghasia katika eneo la vita.

Mazungumzo hayo ya amani yaliyofanyika Jumanne huko Jeddah, Saudi Arabia, yalikuwa ya kwanza rasmi kati ya Marekani na Ukraine tangu malumbano ya wazi yaliyotokea kati ya Zelensky na Rais wa Marekani, Donald Trump, katika Ofisi ya Oval wiki iliyopita.

Katika taarifa ya pamoja, Marekani imetangaza kuwa itaanzisha upya msaada wake wa kijasusi na usalama kwa Ukraine, msaada uliokuwa umesitishwa baada ya mkutano huo wa White House.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa mazungumzo hayo, Waziri Rubio amdsema ana matumaini kuwa Urusi itakubali pendekezo la kusitisha mapigano kwa siku 30, ikiwa ni hatua ya kwanza kuelekea makubaliano ya amani ya kudumu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!