Latest Posts

UKRAINE YADAI KUUTEKA MJI WA KIMKAKATI WA URUSI ENEO LA KURSK

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema vikosi vya nchi yake vimechukua udhibiti kamili wa mji wa kimkakati wa Urusi wa Sudzha katika eneo la Kursk katika uvamizi wao kushtukiza katika ardhi ya Urusi.

Kulingana na Kituo cha Habari cha Aljazeera, Zelenskyy pia amesema siku ya Alhamisi kwamba ofisi ya utawala wa kijeshi inaanzishwa katika mji huo, ambao ulikuwa na watu wapatao 5,000 kabla ya vita ambapo Jenerali Oleksandr Syrsky alisema ofisi hiyo itadumisha sheria na utulivu na “kukidhi mahitaji ya haraka” ya watu katika eneo hilo.

Sudzha ina kituo cha kupimia gesi asilia ya Urusi ambayo inapita kupitia mabomba ya Ukraine hadi Ulaya.

Urusi haikujibu mara moja taarifa ya Zelensky, lakini wizara yake ya ulinzi ilisema mapema Alhamisi kwamba vikosi vya Urusi vilizuia majaribio ya kuchukua jamii zingine kadhaa. Siku ya Jumatano, maafisa wa Urusi pia walikuwa wamekanusha kuwa Ukraine iliuteka mji huo.

Aidha imesema kuwa pia Urusi itatuma wanajeshi zaidi kulinda watu katika eneo hilo

“Kuna vitengo kutoka Wizara ya Ulinzi ya Urusi huko Sudzha wakati adui yuko ndani na karibu na sehemu fulani za mji. Mapigano makali yamekuwa yakifanyika kila siku huko. Adui hawezi kudai udhibiti kamili wa Sudzha kwa sababu (wanajeshi wa Ukraine) hawaidhibiti,” Meja-Jenerali Apty Alaudinov alinukuliwa na shirika la habari la TASS.

Ukraine yenyewe imesema imepata mafanikio zaidi katika uvamizi wake siku ya Alhamisi. Wanajeshi wa Ukraine walikuwa kilomita 35 ndani ya eneo la Kursk, ambapo wanadhibiti eneo la kilomita za mraba 1,150, pamoja na makazi 82, Jenerali wake Syrsky alisema.

Katika siku yake ya 10, huu ni uvamizi mkubwa zaidi wa Ukraine ndani ya Urusi tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi wake mnamo mwaka 2022, lakini Ukraine imesema haina nia ya kuchukua eneo la Urusi badala yake, uvamizi huo ni jaribio la kuishinikiza Moscow kukubali kurejesha amani.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!