Latest Posts

USHIRIKI WA TEA KATIKA BUNGE MARATHON WAONESHA DIRA YA MABADILIKO KWENYE SEKTA YA ELIMU

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Dkt. Leonard Akwilapo @akwilapo , pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Dkt. Erasmus Kipesha @ekipesha1, wameshiriki mbio za Bunge (Bunge Marathon) zilizofanyika leo Aprili 12, 2025. Mbio hizo zilihusisha umbali wa kati ya kilomita 5 hadi 21 na ziliratibiwa na Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tukio hilo limeongozwa na Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, na limehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wabunge, viongozi wa taasisi, mashirika ya umma na binafsi pamoja na wananchi kutoka sehemu mbalimbali. Mbio hizo zililenga kuhamasisha ushiriki wa jamii katika kuunga mkono jitihada za kuboresha sekta ya elimu nchini.

Watumishi mbalimbali kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania nao walijumuika kwenye mbio hizo kama sehemu ya mchango wao katika maendeleo ya elimu. Ushiriki wa TEA katika tukio hili unaonesha dhamira ya dhati ya taasisi hiyo katika kushirikiana na wadau wa maendeleo kuleta mabadiliko chanya katika elimu nchini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!