Latest Posts

UTAFITI WA NDEGE KUFANYIKA KUBAINI WINGI WA MADINI

 

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) inatarajia kufanya utafiti wa kina wa jiofizikia kwa kutumia ndege ili kuongeza eneo la nchi lililofanyiwa utafiti huo kutoka asilimia 16 ya sasa hadi asilimia 34.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa GST Nokta Banteze wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Alhamisi Machi 27, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO, jijini Dodoma.

Banteze amesema utafiti huo unatarajiwa kufanyika katika eneo lenye ukubwa wa asilimia 18 ya eneo lote la nchi yetu, Lengo la Serikali ni kufika asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.

“Utafiti huo ukikamilika utakuwa na manufaa mengi kwa nchi yetu katika sekta za madini, kilimo, maji, mazingira, mipango miji na sekta ya ujenzi”,

Aidha, amesema GST itajenga maabara ya kisasa (state of art labaoratory) katika mkoa wa Dodoma kwa ajili kuimarisha uchunguzi wa sampuli za madini nchini ili kuchochea shughuli za utafiti nchini na hivyo kuhamasisha ukuaji wa Sekta ya Madini.

“Maabara husika itakuwa na vifaa vya kisasa na itaweza kufanya uchunguzi wa sampuli za madini nyingi zaidi ikiwemo zinazojumuisha madini ya kimkakati na madini muhimu”, Ameongeza kwa kusema Banteze.

Hata hivyo Katika kipindi cha miaka minne (2021 – 2025) cha Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, GST imeshuhudia mafanikio makubwa ambayo ni pamoja na Kuongezeka kwa Makusanyo ya ndani  kutoka wastani wa shilingi 1,251,428,472.91 mwaka 2021 hadi shilingi 2,394,211,348 mwaka 2023/2024, sawa na ongezeko la asilimia 91.32.

“Kuongezeka kwa idadi ya sampuli zinazochunguzwa kutoka wastani wa sampuli 19,184 mwaka 2021 hadi sampuli 25,793 mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 34.45. Ongezeko hili limetokana na maboresho makubwa ya maabara yaliyofanyika hasa katika ununuziwa vifaa na mashine za kisasa za uchunguzi wa sampuli,”Amefafanua Banteze.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!