Latest Posts

UTAPELI KWA NJIA YA MTANDAO WAPUNGUA TABORA

 

Mawimbi ya majaribio ya uhalifu na utapeli kwa njia ya mtandao mkoa wa Tabora , yamepungua kutoka majaribio 590 kwa Mwezi Oktoba – Disemba mwaka 2023 mpaka kufikia majaribio 122 kwa mwezi Oktoba – disemba 2024 sawa na upungufu wa asilimia 79.3 kwa mwaka 2023/2024.

 

Taarifa hiyo ilitolewa na Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini( TCRA ) Kanda ya Kati ,Mhandisi. Asajile John , wakati wa ziara ya Naibu waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi , MarryPrisca Mahundi ya ukaguzi wa hali ya Mawasiliano kwa wilaya ya Uyui na Tabora , ambapo amesema kupungua kwa vitendo hivyo kumetokana na utolewaji wa elimu kwa wananchi .

 

“Kwa mkoa wa Tabora tumeona namna mawimbi ya majalibio ya uhalifu yanavyozidi kupungua, matharani kwa mwezi wa Oktoba mpaka disemba mwaka 2023 tulikuwa na majalibio ya uhalifu hapa Tabora lakini katika kipindi cha hicho hicho cha Oktoba – Disemba 2024 yamepungua mpaka 122 sawa na upungufu wa asilimia 79.3%” alisema Asajile.

Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Tabora akiwemo Peter Omenda , Juma Mohamed na Shabani Hamisi, wamesema kuwa utapeli huo umekuwa ujiwaathiri kiuchumi huku wakiomba serikali kuzidisha doria za mtandaoni juu ya matapeli pamoja na kuwachukulia hatua kali za kisheria wanaobainika kufanya hivyo ili kutokomeza vitendo vya utapeli mtandaoni.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!