Latest Posts

UWT WILAYA YA GEITA YAAHIDI KUMUUNGA MKONO DKT. SAMIA KATIKA UCHAGUZI MKUU

Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Geita umeahidi kumuunga mkono mgombea wa urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika uchaguzi mkuu ujao kwa kuhakikisha anapata kura za kutosha.

Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Geita, Paulina Alex, alitoa tamko hilo wakati wa maadhimisho ya kuelekea Siku ya Wanawake yaliyofanyika katika ukumbi wa GEDECO, Geita Mjini.

Amesema kuwa wanatambua jitihada na hatua za maendeleo zilizotekelezwa na Rais Samia tangu aingie madarakani, ambazo ni ishara ya uwezo wake mkubwa wa kuendelea kuiletea Tanzania maendeleo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!