Latest Posts

VETA SIO JAMBO LA KUCHEZEA, NI NJIA YA MAENDELEO

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amesema mafunzo ya ufundi ni muhimu kwa maendeleo ya Watanzania, lakini ni jambo la kusikitisha kuona kuwa bado kuna watu wasiotambua faida za kusoma katika vyuo vya VETA.

 

Mhe. Senyamule ametoa kauli hiyo Machi 24, 2025, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kozi mbalimbali za muda mfupi katika Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kwa ajili ya kikundi cha Wanawake na Samia mkoani Dodoma.

 

“Mafunzo ya ufundi ni muhimu sana kwa Watanzania. Kuna vijana waliomaliza masomo yao katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, lakini baada ya kushindwa kujiajiri wakaamua kutafuta ujuzi kwa kusoma katika vyuo vya VETA,” amesema Mhe. Senyamule.

 

Amewataka wanachama wa kikundi cha Wanawake na Samia kutumia fursa ya mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo wa kujiajiri, kuajiri wengine, au kuajiriwa.

 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Antony Mzee Kasore, amesema kuwa hadi sasa VETA imeshakamilisha ujenzi wa vyuo 29, vikiwemo vyuo vinne vya mikoa na 25 vya wilaya. Aidha, ujenzi wa vyuo vingine 65 umeanza katika maeneo mbalimbali nchini.

 

Naye Mwenyekiti wa Wanawake na Samia, Bi. Fatma Madidi, amesema anaamini kuwa mafunzo hayo yatatoa wataalamu mbalimbali watakaosaidia jamii kwa ujuzi wao.

Hatua hii ni sehemu ya juhudi za kuunga mkono agizo la Serikali la kuhimiza vijana na wasomi nchini kutambua fursa zilizopo katika vyuo vya ufundi stadi ili kujijengea uwezo wa kujiajiri na kuinua uchumi wa taifa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!