Latest Posts

VIKOSI VYA ISRAEL VYAUA WAPALESTINA 48 KWA SAA 24

Maafisa wa Kipalestina wamesema siku ya Jumatatu kuwa vikosi vya Israel vimeua Wapalestina takribani 48 katika saa 24 zilizopita katika Ukanda wa Gaza, walipokuwa wakipigana na wapiganaji wa Hamas, katika wakati ambao madaktari wakiingia katika siku ya pili ya kufanya kampeni ya chanjo ya polio kwa watoto katika eneo hilo.

Maafisa wa Kipalestina na Umoja wa Mataifa wamesema kuwa zaidi ya watoto 80,000 walipatiwa chanjo katika maeneo ya katikati ya Gaza Jumapili, siku ya kwanza ya kampeni hiyo.

Hamas na Israeli wamekubaliana juu ya mapumziko mafupi katika mapigano ili kuruhusu kampeni ya chanjo kwa watoto takriban 640,000 kuendelea. Hakuna uvunjaji wa sheria umetokea karibu na vituo vya chanjo.

Maafisa hao wamesema kuwa Wapalestina saba walifariki katika mashambulizi mawili ya angani ya Israel katika Jiji la Gaza wakati mashambulizi mengine mawili ya namna hiyo yakiua wengine sita katika miji Bureij na Nuseirat.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Reuters, hakukuwa na maelezo ya papo hapo kutoka Israel kutokana na mashambulizi hayo.

Matawi ya makundi ya Hamas na Islamic Jihad wamesema kwamba wapiganaji wao wamekabiliana na vikosi vya Kiyahudi Kaskazini, Kusini na baadhi ya maeneo ya katikati ya Gaza kwa kutumia roketi za kupambana na mizinga.

UNRWA ambalo ni shirika la wakimbizi wa Kipalestina la Umoja wa Mataifa limerudia wito wake wa mapatano ya haraka ya amani ili kuhakikisha kampeni ya chanjo ya polio inafanikiwa na kuwa salama.

Israeli na Hamas wameendelea kutupiana lawama kwa kushindwa kufikia mapatano ya amani ambayo yangeweka kikomo cha vita na kushuhudiwa kurejeshwa kwa mateka wa Kiyahudi na wa kigeni walioshikiliwa Gaza, na Wapalestina wengi walioshikiliwa Israel.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!