Latest Posts

VYAMA VYA USHIRIKA WA MBOGAMBOGA KUNUFAIKA NA SOKO LA KIMATAIFA MARA

Tume ya maendeleo ya ushirika imeanzisha mradi wa uhamasishaji wa uanzishwaji wa vyama vya ushirika wa mazao ya Bustani ikiwemo mbogamboga na matunda lengo likiwa ni kuvisaidia vyama hivyo kupiga hatua na kuuza bidhaa zao kimataifa.

Akizungumzia mpango huo Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani mara Lucas Kihondere amesema mkoa huo una Hoteli nyingi ambazo zinaweza kuuziwa mazao hayo ya matunda na mbogamboga lakini sasa vyama pia vina nafasi ya kuzalisha kwa tija na kuuza kimataifa kutokana na ukweli kwamba soko la ndani limekuwa la kusuasua wakati mwingine.

“Mkoa wa Mara tuko mpakani na nchi ya Kenya, na hapa kupitia Sirari kama vyama vya ushirika vikiweza kuzalisha kwa tija wanaweza kuuza matunda na mbogamboga upande wa Kenya kwa hiyo tunahitaji ushirika ujitanue katika biashara” Amesema Kihondere.

Pia, amewataka kutumia watalaamu wa kilimo ili kuhakikisha wanapata mazao bora na ambayo yanaweza kuingia katika ushindani wa soko la kimataifa badala kuangalia masoko ya ndani pekee.

Baadhi ya wanufaika wa mafunzo hayo akiwemo Masumbuko Mabasa kutoka ‘GOHOMACOS’ amesema kuwepo na soko la uhakika pamoja na uboreshaji wa skimu za umwagiliaji kutasaidia kwa kiasi kikubwa kufikia malengo ya wakulima hususani katika eneo hilo la  mbogamboga na matunda hivyo wameiomba serikali kutoa kipaumbele katika eneo hilo.

Afisa ushirika kutoka tume ya maendeleo ya ushirika Ramadhan Miraji amesema mafunzo hayo kwa wajumbe wa bodi lengo lake ni kuwajengea uwezo wa kutambua majukumu yao pamoja na taratibu na sheria za vyama vya ushirika, namna ya kusimamia shughuli za chama ikiwa pamoja na Kupata masomo kwa mazao yanayozalishwa na wanachama wao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!