Latest Posts

WACHIMBAJI WAKUMBUSHWA KUTOTUMIKA KISIASA WAKATI WA UCHAGUZI

Wachimbaji wadogo wa madini mkoani Mara wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, huku wakihimizwa kutojihusisha na vitendo vya wanasiasa wenye malengo ya kuvuruga amani ya taifa.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Soya One Limited, Bw. Chacha Soya, alipokuwa akizungumza na Jambo TV. Ameitaka jamii ya wachimbaji kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi na kujiepusha na ushawishi wa kisiasa unaolenga kuvuruga utulivu wa nchi.

Soya alisisitiza kuwa wachimbaji wana jukumu kubwa la kushirikiana na Serikali kulinda amani na kushirikiana na viongozi wa dini kupinga mienendo inayokwenda kinyume na maadili na tamaduni za Kitanzania.

“Serikali imekuwa karibu sana na wachimbaji wadogo na imetuwekea mazingira bora ya uchimbaji. Tunapaswa kuiunga mkono na kukataa vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani tunapoelekea uchaguzi,” alisema Soya.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Chikoka, aliwataka wakazi wa Mara kushiriki kwa amani na kuhakikisha kila mmoja anakuwa mlinzi wa mwenzake, huku wakikataa upotoshaji dhidi ya viongozi wa kitaifa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!