Vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya kijeshi ya kujitolea Operasheni ya miaka sitini ya Muungano katika kikosi cha Jeshi 823 Msange JKT iliyopo mkoani Tabora wametangaziwa na Jeshi la kujenga Taifa JKT kujiunga kwenye kambi za kujifunza mafunzo ya Ufundi stadi ili kuwajengea uwezo wa kulitimikia Taifa katika nyanja mbalimbali na kujikwamua kiuchumi.
Kauli hiyo imetolewa Leo April 11, 2025 na Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, Kanali Projest Rutaihiwa wakati wa kufunga hayo yaliyofanyika kwa muda wa miezi Minne kambini hapo.
Kwa Upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Gerald Mongella amewataka vijana waliohitimu mafunzo hayo kukiishi kiapo cha utilii walicho apa katika kuwa msitari wa mbele kuilinda amani ya nchi.
Nae, Kamanda wa kikosi hicho cha 823 KJ Msange JKT Kanali Sadick Mihayo amewasisitiza wahitimu hao kuwa waadilifu na kutokujihusisha na vitendo viovu kwani vijana ndo nguvu kazi ya Taifa katika kupigania amani ya nchi pamoja na kukuza uchumi.
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo wamebainisha kuwa mafunzo ya ufundi stadi yatakuwa mwarobaini kwao katika kujikwamua kiuchumi.