Latest Posts

WAKAZI WANNE WA SAME MAHAKAMANI KWA KESI YA UHUJUMU UCHUMI

Wakazi wanne wa Wilaya ya Same wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi zenye uzito wa kilogramu 518.57.

Watuhumiwa hao, Nimkaza Mbwambo, Prosper Lema, Nterindwa Mgalle, na Stephanie Mrutu, walisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Ally Mkama. Wakili wa Serikali, Julieth Komba, alidai kuwa Machi 21, 2025, watuhumiwa walitenda makosa hayo katika kijiji cha Rikweni, Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa mashtaka, Nimkaza Mbwambo alikamatwa akisafirisha kilogramu 138.58 za mirungi, Prosper Lema kilogramu 113.29, Nterindwa Mgalle kilogramu 160.25, na Stephanie Mrutu kilogramu 106.45.

Wakili wa serikali alieleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 11, 2025, kwa kutajwa, huku watuhumiwa wote wakiendelea kushikiliwa mahabusu.

Wakazi wawili wa Wilaya ya Same, Dorisiana Mchome na Aisha Mbaga, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Same wakikabiliwa na shtaka la kusafirisha kilogramu 54.15 za mirungi.

Wakili wa Serikali, Michael Matowo, aliiambia mahakama kuwa Machi 21, 2025, katika kijiji cha Rikweni, Dorisiana Mchome alikamatwa akiwa na kilogramu 17 za mirungi, huku Aisha Mbaga akikamatwa na kilogramu 37.15.

Matowo alibainisha kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 10, 2025, kwa kutajwa, huku watuhumiwa wakiendelea kushikiliwa mahabusu. Hata hivyo, Dorisiana Mchome anaweza kupata dhamana iwapo atatimiza masharti, ingawa wadhamini wake bado hawajatoa taarifa sahihi mahakamani.

Operesheni maalum iliyofanyika kati ya Machi 19 na 25, 2025, iliwakumba watu kadhaa wilayani Same, akiwemo Interindwa Kirumbi, maarufu kama “Mama Dangote,” anayedaiwa kuwa kinara wa biashara ya mirungi.

Operesheni hiyo pia ilibaini na kuteketeza mashamba ya mirungi yenye jumla ya ekari 285.5, hatua ambayo inatajwa kuwa sehemu ya juhudi za serikali kudhibiti biashara haramu ya dawa za kulevya nchini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!