Wakulima Wadogo wamesema ukosefu wa Elimu kwa jamii kuhusu mchakato wa uandaji wa bajeti hasa kwenye sekta ya Kilimo umepelekea kutengwa na serikali katika suala hilo nakuitaka kuendelea kutoa Elimu kwa Wananchi.
Wakulima hao wametoa maoni hayo katika Maazimio yao kwenye Mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika la ActionAid Tanzania katika mradi wa Transformative Impact Fund (TIF), wawakilishi wa wakulima kutoka wilaya ya Chamwino na Halmashauri ya Singida.
Aidha wamesema Kutokushirikishwa katika uandaaji wa bajeti kunapelekea kukosa haki yao ya msingi hasa kuhoji mapato na matumizi ya Halmashauri.