Latest Posts

WALIMU KISARAWE WADAI MALIMBIKIZO YA MISHAHARA, MADENI SUGU YA LIKIZO

Chama cha Walimu CWT Wilaya ya Kisarawe kimelalamikia malimbikizo ya stahiki Walimu  kutolipwa kwa muda mrefu licha ya jitihada za chama hicho kuwasilisha madai hayo kwa mamlaka husika.

Madai hayo yamewasilishwa na Katibu wa Chama cha Walimu CWT Wilayani humo Mwalimu Tebe Mashine Tebe wakati akisoma taarifa ya utendaji wa chama hicho katika mkutano mkuu kwa kipindi cha  Januari 2020 hadi Disemba 2024.

Mwalimu Tebe amesema jumla ya Walimu 250 wanadai madeni ya uhamisho, Walimu 70 wanadai malimbizo ya mishahara huku walimu wengine wakidai madeni  Sugu ya likizo.

Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Sara Ngwele  ambaye ndiye mkuu Utumishi amesema kama halmashauri wataunda kamati ya kutathmini madai hayo ya walimu pamoja na kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaochelewesha taarifa za walimu kufika kwenye mamlaka husika ili ziwafanyiwe kazi hali inayopelekea ucheleweshaji katika utatuzi wa madai hayo ya Walimu.

Katika hatua nyingine mkutano huo uliambatana na uchaguzi wa uongozi upya wa CWT ngazi ya Wilaya hiyo uliyosimamiwa na Katibu wa CWT Mkoani wa Pwani Susan Shesha.

Akitangaza Matokeo ya Safu ya Uongozi Mpya, Bi. Shesha amemtaka Mwenyekiti mteule wa CWT Wilaya ya Kisarawe Mwalimu Francis Mkamba aliyetetea nafasi hiyo kwenda kupigania haki na madai za Walimu Wilayani humo.

Kwa upande wake Mwenyekiti Mleule Mwalimu Mkamba aliyewashinda wenzake watatu kwa kupata kura 59 kati ya kura 117 ameahidi kwenda kushughulikia madai ya Walimu kupata stahiki zao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!