Latest Posts

WALIMU WANADAI ZAIDI YA BIL.10, ‘TABIA YA KUVAMIA MISHAHARA YA WALIMU IKOME’: CHAKAMWATA

 

Na Josea Sinkala, Mbeya.

Chama cha kutetea haki na maslahi ya walimu Tanzania (CHAKAMWATA), kimetangaza kutua mahakamani kuzishtaki Halmashauri mbalimbali nchini kwa madai ya kushindwa kulipa stahiki za watumishi wa kada ya ualimu kwa kushirikiana na Chama Cha walimu CWT kwa madai ya zaidi ya shilingi billion 12.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya Aprili 08, 2025, katibu mkuu wa Chama cha kutetea haki na maslahi ya walimu nchini (CHAKAMWATA) mwalimu Meshack Kapange, amesema Halmashauri mbalimbali nchini Tanzania zinadaiwa na walimu lakini hadi sasa hakuna malipo yoyote yaliyotolewa ambapo chama cha walimu Tanzania CWT kwa kushirikiana na Halmashauri mbalimbali nchini isipokuwa mkoa wa Singida pekee, zinadaiwa mabillion ya fedha.

“Na sisi CHAKAMWATA tumefuatilia kwa kina ili TAMISEMI itoe maelekezo kwa mamlaka zake za chini lakini hakuna chochote kilichofanyika, walimu wananyanyaswa kwa kuingiziwa makato ya Chama cha walimu bila ridhaa yao, walimu hatuko huru”, amesema Kapange, katibu mkuu wa CHAKAMWATA Taifa.

Kutokana na madai hayo amesema chama cha kutetea haki na maslahi ya walimu Tanzania kimepanga kuchukua hatua za kwenda mahakamani kufungua kesi ikizingatiwa katika mikoa yote Tanzania ni mkoa wa Singida pekee yake ambao hauna shida na Chama cha kutetea haki na maslahi ya walimu CHAKAMWATA.

Pia ameeleza kuwa kwa zaidi ya miaka 30 walimu wamekuwa wakilazimishwa kujiunga na Chama cha walimu Tanzania (CWT) na kwamba walimu hao wamekuwa wkaikumbana na maonezi mbalimbali ikiwemo kuingiziwa makato ya CWT bila ridhaa ya walimu.

“Kuingiza makato kwenye mshahara wa mfanyakazi kinyume Cha ridhaa yake ni kosa la jinai. Sheria ya ajira na mahusiano kazini kifungu cha 28 kinakataza mwajiri kuingiza makato kwenye mshahara wa mfanyakazi bila mfanyakazi kuridhia labda hayo makato yawe ya lazima kama vile makato ya kodi ya Serikali lakini mengine ni lazima mfanyakazi aridhie”, amesema katibu mkuu huyo na kuongeza.

“Kutokana na hayo yote, tumeorodhesha mikoa yotena wilaya zote, tuna Halmashauri 125 nchi nzima katika, ni mkoa wa Singida peke yake ndio hauna nongwa na CHAKAMWATA na tumeorodhesha pesa ya mwalimu aliyokata katika wanachama kumi na mbili elfu mia mbili thelathini na moja asilimia moja ya CWT na asilimia moja ya CHAKAMWATA tunakwenda mahakamani kufungua kesi na kabla ya kufungua kesi tumeshawapekea waajiri wote nchi nzima barua ya notice (kusudio la kuwashtaki) na wanatakiwa kutujibu ndani ya siku 30 na tunawadai jumla ya shilingi billion 12 million 326 laki tisa na sitini elfu na 571 na senti tisini. Hizi fedha wanatakiwa kulipa CWT na wanatakiwa kushirikiana na hao waajiri kwasababu anayeingia kwenye mishahara ni mwajiri halafu anampelekea CWT (Chama cha walimu). Kwanini Serikali kuu itoe maelekezo lakini TAMISEMI ikiuke maelekezo, Halmashauri zikiuke maelekezo ndio maana nchi haiendelei kwasababu kuna kutokuwepo kwa nidhamu kwenye mifumo yetu ya utawala na mifumo yetu ya uongozi”, ameeleza katibu mkuu wa CHAKAMWATA Taifa Mwalimu Meshack Kapange.

Kiongozi huyo mtendaji amekemea tabia ya kukata makato ya mishahara ya watumishi hasa walimu bila kuwashirikisha.

“Tunataka hii tabia ya kuvamia mishahara ya wafanyakazi hasa walimu ikome. Kazi ni mali ya mwajiri lakini mshahara ni mali ya mtumishi tena unamlipa kwa deni maana amekutumikia kwa mwezi mzima unamlipa baada ya kukutumikia, ni deni anakudai halafu unaenda unalikata”, ameongeza Mwal. Kapange.

Baadhi ya walimu wanasema waliamua kujiunga na chama cha kutetea haki na maslahi ya walimu Tanzania (CHAKAMWATA) kwasababu kimekuwa kikitetea maslahi yao bila kujali wameajiriwa au hawajajiriwa na kuwa sio chama cha ubinafsi na kina makato ya asilimia moja pekee kwa walimu hao.

Wamesema wanasubiri mwezi mmoja wa barua waliyoitoa ili kutaka malipo kwa walimu ya zaidi ya shilingi billion 12 lasivyo wataenda mahakamani kushtaki ili walimu kupata stahiki zao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!