Latest Posts

WANAHABARI WANAWAKE MWANZA WATAKA MADAWATI YA JINSIA KWENYE VYOMBO VYA HABARI

 

Waandishi wa habari wanawake Mkoa wa Mwanza wameomba kuundwa kwa madawati ya jinsia kwenye vyombo vya habari mahususi kwa ajili ya kushughulikia matukio ya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanahabari.

Wakizungumza leo Aprili 15, 2025 kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari juu ya ukatili dhidi ya wanawake Waandishi wa habari na wanahabari yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu (UNESCO).

Wanahabari hao wamesema wanaimani kikiwepo chombo kama hicho ambacho kitakuwa kinajitegemea itasaidia kupunguza matukio hao kwa wanahabari.

“Wakati mwingine unakuta bosi wako anakuhitaji kimahusiano unapokataa anakutishia kukufukuza kazi sasa kutokana na unyanyasaji huo wa kingono unapelekea wakati mwingine sisi waandishi wa habari wa kike tunashindwa kufanyakazi ipasavyo na kutekeleza majukumu yetu ipasavyo lakini pia hii imepelekea kuwepo kwa idadi ndogo ya wanawake kwenye vyombo vya habari,” amesema Chausiku Saidi mwandishi wa habari kutoka Matukio Daima

Akiunga hoja hiyo Mwandishi wa Habari kutoka Redio Saut Fm, Riziki Lukumai amesema wanawake wanaonekana kama chombo dhaifu kwenye vyombo vya habari hali inayopelekea kukumbana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.

“Mimi ningeshauri kuanzishwe dawati la jinsia la kushughulikia changamoto za Waandishi wa habari wanawake na wanaume wanazokumbana nazo kwenye nyombo vya habari na mitandaoni ambako watakuwa wanaenda kuripoti na kufanyiwa kazi,” amesema Riziki

Kwa upande wake, Farhia Rashidi mwandishi wa habari kutoka redio Saut Fm ametaka usawa kwenye vyombo vya habari hali itakayopelekea kila mtu kupewa sawa bila kujali jinsia.

“Nimegundua ukatili upo na tunafanyiwa mfano kubaguliwa na kuonekana sisi hatuna usawa kwa maana ya kama mwanaume anapewa hiki na mwanamke apewe hicho kwa sasa vyombo vya habari vingi havitendi usawa,” amesema Farhia

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi Mkoa wa Mwanza (MPC), Edwin Soko amesema japokuwa hamna takwimu za moja kwa moja zinazoonyesha ukubwa wa tatizo hilo haiondoi kwamba changamoto hiyo ni kubwa katika vyombo vya habari.

“Kwanza tafiti zinakiri upo na vilevile ni mkubwa kwahiyo tunaamini kama ni hivyo lazima tutumie njia madhubuti na tuwe na mpangokazi wa kuhakikisha tunawafundisha waandishi hawa namna ya kukabiliana na matukio hayo ikiwa ni pamoja na kuwa na sera ya jinsia na kuwa na madawati ya jinsia,” amesema Soko

Akizungumzia mafunzo hayo Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano na Habari kutoka Tume ya Taifa ya UNESCO, Christina Musaroche amesema mafunzo hayo yamejikita katika kuhamasisha uzingatiaji wa kanuni na maadili bora yanayomlinda mwanawake mwandishi wa habari dhidi ya unyanyaswaji anapotekeleza majukumu yake.

“Ni ukweli usiopingika kuwa ukatili dhidi ya wanawake waandishi wa habari umekuwa mjadala sio tu nchini Tanzania bali hata duniani kote. Ukatili dhidi ya wanawake waandishi wa habari ni ishara ya unyanyapaa na unaweza kusababisha madhara mbalimbali kama vile kuongezeka kwa msongo wa mawazo, wasiwasi, mfadhaiko, na woga wa kujihusisha na mijadala muhimu ya umma, kutojiamini katika kutoa maoni, yote haya yakichochewa na kuhofia kutendewa ukatili zaidi,” amesema.

Ameongeza kuwa “Unyanyasaji wa wanawake waandishi wa habari, iwe kwenye Vyumba vha Habari au nje, unasababisha pamoja na mambo mengine kukosekana kwa ari ya kupenda kazi na madhara mengine ambayo hatimaye yanaweza kuathiri ubora wa kazi zinazofanywa na wanawake waandishi wa habari,”.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!