Latest Posts

WANANCHI WA HIMIZWA KUENDELEA KUITUNZA NA KUIDUMISHA AMANI YA NCHI

 

Na Theophilida Felician.

Rais wa taasisi ya INTERNATIONAL PEACE INFOMATION I.P.I na mwanzilishi wa taasisi ya umoja wa amani kwanza Prf Wilson George Munguza ametoa wito akiwahamasisha wananchi kuendelea kuitunza amani ya nchi iliyodumu kwa muda murefu.

Akizungumza na Blog hii Aprili 5, 2025 makao makuu ya ofisi za taasisi hiyo Temeke mkoani Dare es salaam amebainisha kwamba bila ya amani kila jambo litakwama hivyo ni wajibu wakila mtu kusimama imara katika hilo hususani kipindi hiki tunachoelekea uchaguzi mkuu wa Urais, ubunge na udiwani.

Amefafanua kwamba wao kama taasisi wamejipanga vyema kuhakikisha elimu ya amani inawafikia wananchi kama inavyofanya kwa sasa nchi mbalimbali zikiwemo nchi za Afrika mashariki.

Ameishukuru serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna inavyoonyesha ushirikiano kwa taasisi hiyo katika kuitunza amani.

Naye Rais wa umoja wa amani kwanza kutokea DRC KONGO Maliyamungu Justin Nvunyibwa amesema licha ya nchi hiyo kuzipitia changamoto za ukosefu wa usalama baadhi ya maeneo bado wanaendelea na juhudi za kueneza elimu ya amani nchini humo.

Hata hivyo amempongenza Rais wa INTERNATIONAL PEACE INFOMATION I.P.I na mwanzilishi wa taasisi ya umoja wa amani kwanza Prf Wilson George Munguza kwa namna anavyopambana na kuwapa ushirikiano katika utendaji kazi wao huko KONGO.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!