Latest Posts

WANANCHI WA MTWARA WASISITIZWA KUEPUKA MAKUNDI NA KULINDA AMANI YA TAIFA

Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Jamaldin Salim amewaagiza viongozi wote wa dini ya kiislamu kujitahidi kuomba dua mara kwa mara ili Mwenyenzi Mungu aweze kulivusha salama Taifa hasa wanapoelekea kipindi cha uchaguzi mkuu Oktoba 2025.

Ametoa agizo hilo kwenye Iftari na dua maalumu ya kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala na kuratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara iliyowakutanisha watu zaidi ya elfu 4,000.

Pia amewataka waumini wa dini hiyo na jamii kwa ujumla wajitahidi kuepuka jambo lolote ambalo wanaona linaashilia kuchochea vurugu ndani ya nchi ili kuepuka changamoto ambazo zinatokea kwa baadhi ya nchi jirani.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amesema kuwa ipo haja ya kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan kwakuwa yapo mambo mengi ambayo yametekelezwa ndani ya kipindi cha miaka minne ya uongozi wake ikiwa ni pamoja na uborehsaji wa bandari ya Mtwara ambayo imepelekea wakazi wa mtwara kunufaika kwa kupata ajira mbalimbali.

Pia amewataka wananchi kutokubali kutenganishwa na makundi mbalimbali yanayoweza kujitokeza kuelekea kipindi cha uchaguzi huo.

“Jambo lingine waendelee kuitunza amani na utulivu kwenye mkoa ili kuendelea kuwa na maendeleo kwani bila amani hakuna maendeleo yanayopatikana na amewaomba kukubali kuwa na maridhiano inapotokea tofauti yoyote ili kuepuka kuvunja amani”amesema Sawala

Makamu wa Askofu Jimbo Katoliki Mtwara Parokia ya Watakatifu wote Fr Patrick Mwaya ametoa rai kuelekea uchaguzi mkuu huo kwa kuhakikisha wanachagua viongozi wanaostahiki ili waendelee kudumisha, kulinda, kutunza na kuiombea amani iliyopo na kumuombea Rais ili aweze kuongoza kwa hekima na busara.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!