Latest Posts

WANAWAKE WA GEUWASA WAJITOLEA KUWAFARIJI WAFUNGWA WA KIKE GEITA

Wafanyakazi wanawake wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Geita (GEUWASA) leo wameadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani kwa kutoa misaada mbalimbali kwa wafungwa wa Gereza la Wanawake Wilayani Geita. Katika tukio hilo, wameikumbusha jamii juu ya umuhimu wa kuwapenda na kuwathamini watu waliopo gerezani, licha ya makosa waliyofanya.

Wanawake hao walipowasili gerezani waliwakabidhi zawadi na mahitaji mbalimbali kwa wanawake wenzao waliopo kifungoni. Wakizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo, walisema wameamua kusherehekea siku hiyo kwa kutoa upendo kwa wenzao kama ishara ya mshikamano na kuthamini utu wa kila mwanamke.

Kwa upande wake, Mkaguzi Msaidizi wa Gereza la Wanawake Geita, Joyce Jonas, amewashukuru wanawake wa GEUWASA kwa moyo wao wa huruma na kwa kuwapelekea zawadi muhimu kwa wanawake waliopo gerezani.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanafanyika leo, Machi 8, kwa kaulimbiu inayosema: “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji.”

Kaulimbiu hii inalenga kuhimiza jamii kuhusu umuhimu wa kuimarisha usawa wa kijinsia kwa wanawake na wasichana kwa kuhakikisha wanapata fursa sawa katika sekta zote za maisha, ikiwemo elimu, uchumi, uongozi na afya. Pia inasisitiza uwezeshaji wa wanawake kwa kuwapa nafasi za kushiriki katika maamuzi muhimu ya kijamii na kiuchumi ili kujenga jamii yenye haki na maendeleo endelevu.

Wanawake wa GEUWASA wamesema kuwa utekelezaji wa kaulimbiu hii unahitaji mshikamano wa jamii nzima katika kuwawezesha wanawake na wasichana kufikia ndoto zao bila ubaguzi wowote.

 

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!