Latest Posts

WATIA NIA 44 WANAWAKE WACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE MTWARA

Jumla ya watia nia 44 wanawake wamechukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi Mkoani Mtwara ikiwemo Ubunge, Ubunge Viti Maalum pamoja na Ubunge Viti Maalum Vijana Tanzania Bara.

Akitoa taarifa za watia nia wa nafasi hizo katika majimbo 10 yaliyopo mkoani Mtwara Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo Juma Hassan amesema kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2025 wanawake hao 44 waliyochukua fomu 24 ni wale wa kugombea Ubunge kwenye majimbo,18 Ubunge wa Viti Maalum na kwa upande wa wagombea Ubunge Viti Maalum Vijana Tanzania Bara ni wanawake 2 ambao ni Rehema Lukundu na Shakila Mpomo.

Amefafanua kuwa idadi ya watia nia hao wa nafasi ya ubunge katika majimbo 10 mkoani humo ikiwemo Jimbo la Tandahimba ambapo wanawake 2 wamechukua fomu kati ya wanaume 14, Mtwara Mjini wanawake 3 ikiwemo Judith Nguli kati ya wanaume 9 akiwemo Hassan Mtenga anaetetea kiti chake,Mohamed Abdallah (Mudy Ray) na Joel Nanauka.

Aidha Mtwara vijijini wanawake 3 akiwemo Hawa Ghasia aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo na wanaume 5 akiwemo Arif Premji, Nanyamba mwanamke 1 kati ya wanaume 4,Newala mjini wanawake 3 kati ya wanaume 7 akiwemo Haruni Maarifa,Newala vijijini wanawake 2 kati ya wanaume 8.

Na Nanyumbu wanawake 2 kati ya wanaume 7,Lulindi wanawake 3 kati ya wanaume 9 akiwemo Issa Mchungahela na Sameer Murji,Masasi Mji wanawake 3 na wanaume 5 ambapo Geoffrey Mwambe anatetea kiti chake na Ndanda wanawake 2 kati ya wanaume 9 akiwemo Cecil Mwambe.

Idadi hiyo inafanya jumla ya watu waliyochukua fomu na kurejesha ni 98 wakiwemo wanaume 74 na wanawake 24,ubunge viti maalum 18 na wagombea ubunge kundi la umoja wa vijana ccm 2 na kufanya jumla ya watia nia wanawake 44 kuanzia juni 28 mpaka julai 2,2025.

Pia Katibu huyo amewashukuru wanachama wote kwa kutimiza wajibu wao wa kuchaguliwa na kuchagua kama wanaachama wa chama hicho

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!