Na Helena Magabe-Tarime
Jumla ya watiania 28 waliojitosa kuwania ubunge Wilayani Tarime tayari wote wamekwishajaza na kurejesha fomu zao katika ofisi ya CCM Wilaya ya Tarime kwaajili ya mchakato mwingine unaufuata ambapo Katibu wa CCM Wilaya amesema kuwa ni kwa mara ya kwanza Tarime zoezi la uchukuaji fomu limekuwa la utulivu na amani kwasababu lilikuwa huru na haki..
Akizungumza na Wandishi wa Habari, Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime Hamza Adamu Kyeibanja amesema wagombea katika Jimbo la Tarime Vijijini ni 14 wanaume ni 10 na wanawake ni wawili 2 na kwa upande wa jimbo la Tarime Mjini ni watia vile vile ni 14 ambapo wanaume ni kumi 10 na wanawake ni wawili 2 hivyo Wanaume jumla ni 20 na Wanawake ni wanne 4.
Kyeibanja amesema jumla ya watia 28 waliochukua fomu za kuwania ubunge wote wamerejesha fomu hizo zikiwa zimejazwa ambapo kila Mtia nia alilipia fomu yake shilingi laki tano 500,000 pesa ambayo ililipwa kwenye control number na hakukuwa na malalamiko yoyote wala manung’uniko hivyo zoezi lilianza vizuri na kumalizika leo saa 10 kamili jioni vizuri bila shida.
”hata sisi tumeshangaa imekuwaje idadi imelingana kwa upande wa wanaume na wanawake kwa majimbo yote ila nashukuru Mungu zoezi limeisha vizuri bila changamoto yoyote hakukuwa na malalamiko yoteyote tuliomba tuanze salama na tumalize salama ” alisema Kyeibanja
Amesema kuwa tangu siku ya kwanza juni 28,2025 zoezi la kuchukua fomu lilipoanza hadi julai 2,2025 Ofisi ilikuwa ikifunguliwa saa 1 asubuhi na zoezi la kusajili watia lilikuwa lilianza saa 2:00 hadi saa 10:00 jioni, VIle vile Watia nia waliitikia wito wa zuio la kufata fomu na msululu wa watu au wapambe isipokuwa waliambatana na Waandishi wa habari mmoja mmoja au Wawili au zaidi lakini hakukuwepo na umati wa watu.
Aidha amewashukuru wananchi na watia nia kwa utulivu ambapo amesema kwa sasa vikao vinavyotakiwa kuendelea ni vya kikatiba tu hairuhusi mtu kuendesha vikao tofauti na kuongeza kuwa jumla ya kata zitakazo shiriki uchaguzi ni 35 ,Tarime vijijini 27 na Tarime Mjini kata 8 ambapo amewaomba Waandishi wa habari kuhamasisha amani na utulivu uendelee kuwepo hadi uchaguzi mkuu.