Latest Posts

WATOTO 126 WENYE ULEMAVU MUSOMA WAPATIWA BIMA ZA AFYA

Watoto 126 wenye mahitaji maalum katika Wilaya ya Musoma Mkoani Mara wamekabidhiwa Bima za Afya ili kuwaondolea changamoto ya huduma za matibabu pindi wanapohitaji huduma za matibabu

Bima hizo za CHF zimetolewa na Shirika lisilo la kiserikali la St Justin Foundation kwa kushirikiana na Conrad Hilton fund for Sister ambapo wamesema watoto hao baada ya kuibuliwa kutoka majumbani walibaini kuwa na changamoto ya ukosefu wa huduma za Afya kutokana na maisha wanayoishi kwenye jamii.

Akizungumzia hali hiyo Meneja Mradi wa Shirika hilo Nollasko Mgimba Alisema waliibua kutoka majumbani watoto 189 waliokuwa wamefichwa na wazazi wao sasa wamekabidhiwa Bima za Afya kwa watoto 126 ili kuwasaidia kupata matibabu.

Mbali na bima hizo za Afya, Shirika la St Justin Foundation wamekabidhi nguo za shule madaftari na kalamu kwa wanafunzi hao wenye uhitaji

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!