Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa zaidi ya 60 kwa makosa mbalimbali ya uhalifu kwa kipindi cha Mwezi Januari na machi 2025 katika operesheni, doria na misako ambayo imekuwa ikifanywa na Jeshi hilo ikiwa ni mpango mkakati wa kukabiliana na matukio ya uhalifu katika mkoa wa Tabora.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora .SACP Richard Abwao Machi 29, 2025.
Kamanda Abwao ,amebainisha Watu humiwa wa matukio hayo ni pamoja na wizi wa piki piki, Matumizi ya noti bandia , Matumizi ya madawa ya kulevya aina ya bangi , watengenezaji wa Pombe moshi aina ya Gongo , Matumizi ya silaha za moto aina ya Gobole ambazo zilikuwa zikitumika katika matukio ya uhalifu pamoja makosa ya unyanyasaji wa kijinsia .
Aidha, Kamanda Abwao, amewataka wananchi mkoani Tabora kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kukabiliana na uhalifu na wahalifu .