Latest Posts

WATUMISHI WA TEA WAJENGEWA UELEWA KUHUSU TAHADHARI NA KUKABILIANA NA MATUKIO YA MOTO

 

Watumishi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wamepatiwa elimu kuhusu mbinu za kujikinga na kuchukua tahadhari dhidi ya matukio ya moto ikiwa ni mfukikizo wa siku tatu za mafunzo ya ndani yaliyoanza tarehe 36 Mei, 2025.

Mafunzo hayo yametolewa na Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Bw. Stephen Kette, katika ofisi za TEA zilizopo Ilazo, Jijini Dodoma.

Kupitia mafunzo hayo, watumishi wa TEA wamepata fursa ya kujifunza kuhusu: aina za mioto, sababu zinazosababisha matukio ya moto, njia sahihi za kuzuia moto, hatua za kuchukua pindi ajali ya moto inapotokea, na namna ya kutumia vifaa vya kuzimia moto kwa usalama.

Mafunzo haya ni sehemu ya jitihada za TEA katika kujenga mazingira salama ya kazi kwa watumishi wake na kuimarisha utayari wa kukabiliana na dharura mahali pa kazi.

#EmergencyPreparedness#WorkplaceSafety
#

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!